Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Ayubu Sebabili ameyasema hayo leo akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kata kwa kata ambapo siku ya leo ametembelea kata za Mtindiro, Kwabada na Kwakifua zote zilizopo tarafa ya Muheza.
Akiwa katika ziara hiyo ambayo anaitumia kusikiliza kero za wananchi, suala la changamoto ya wanafunzi kutoripoti shuleni kwakisingizio cha wazazi kukosa fedha zakuwanunulia watoto sare za shule lilijitokeza na kupelekea Mkuu wa Wilaya kutoa kauli hiyo.
“Mwanafunzi kukosa sare za shule kisiwe kisingizio chakutoripoti shuleni katika kipindi hichi ambacho shule zimefunguliwa kuanzia leo, hivyo basi naagiza wanafunzi wote ambao hawana sare hadi sasa wapokelewe bila kuzuiliwa, natoa mwezi mmoja na baada ya hapo mzazi ambae atakua hajatekeleza wajibu wake kwa mtoto wake tutamchukulia hatua” alisema Mhe. Sebabili.
Aidha changamoto mbalimbali zilitolewa na wananchi katika kata hizo ambapo kero za ukosefu wa watumishi wakutosha katika sekta za elimu na afya, majengo chakavu ya shule, maji na miundombinu mibovu ya barabara zimekua kero zilizojitokeza zaidi na huku zikitolewa ufafanuzi na waatalamu wa halmashauri ambao waliambatana na Mkuu wa Wilaya katika ziara hiyo.
Zaidi katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya Mhe. Ayubu Sebabili amewashukuru wananchi kwakushiriki vyema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ambapo zoezi zima lilifanyika kwa amani na utulivu mwanzo hadi mwisho bila kua na dosari ya aina yeyote nakuwataka wananchi wanahakikisha amani hiyo wanaitunza kwa nguvu zote.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.