Sunday 15th, December 2024
@OFISI YA KATA MBARAMO
Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani hufanyika kila Desemba 01 ya Kila Mwaka yakiwa na lengo la kuikumbusha jamii juu ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na namna ya kujikinga na ugonjwa huo.
Madhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani kwa Mwaka huu Wilayani Muheza yatafanyika Siku ya Alhamisi mnamo Desemba 1 katika ofisi ya kata ya Mbaramo kuanzia saa 3:00 asubuhi ykiongozwa na Kaulimbiu isemayo “IMARISHA USAWA”ikiweka msisitizo wa wa kuhakikisha hakuna vikwazo vya Kiusawa katika jamii ikiwemo Usawa wa Kijinsia na Usawa katika huduma na haki za binadamu kwa Ujumla.
Mgeni rasmi katika Maadhimisha hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Halima Abdallah Bulembo amabye ataongoza hafla hiyo.
Katika Maadhimisho hayo kutakuwa na shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo Utoaji elimu ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Elimu ya Mtumizi ya Madawa ya Kulevya, Lishe, Ujasiriamali na Upimaji wa hiari wa VVU (Virusi vya Ukimwi).
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.